NDOA YA SANDRA WA BONGO MOVIE YASAMBARATIKA.......

NDOA ya mwanadada anayeendesha maisha yake kwa kucheza filamu, Salma Salim ‘Sandra’ inadaiwa kusambaratika.Sandra aliyeolewa na mwanaume aliyefahamika kwa jina la Haisam na kufanikiwa kupata watoto wawili, inadaiwa ndoa yao imefikia ukingoni kutokana na wawili hao kutofautiana.Akizungumza na Mwandishi wetu, mmoja wa ndugu wa mwanaume aliyeomba jina lake lisiandikwe mtandaoni alisema, wawili hao waliachana hivi karibuni baada ya kuona ndoa yao ‘inanyevuliwa’.
“Ni kweli wameshindwana na sasa kila mmoja yuko kivyake,”
alisema ndugu huyo.

Sandra alipotafutwa kuzungumzia hilo hakuwa tayari kutoa ushirikiano, mumewe hakuweza kupatikana ila mdogo wa mume ambaye ni Miss Tanzania 2012, Salha Israel alikiri ndoa ya kaka yake kusambaratika.