PROFESA J AMPA SHAVU DIAMOND......"DOGO NDO KWANZA ANAFANYA VEMA "


Diamond bado ana ng'aa na  utemi wake umeendelea kudumu kwa miaka miwili mfululizo sasa. Kuanzia show zake, uvaaji wake mpaka nyimbo zake mpya zinapotoka hapakosekani mengi ya kuzungumziwa kuhusiana na msanii huyu kipenzi cha wengi.Akiwa na video mpya hewani, Nataka Kulewa, bado jina la Diamond limeendelea kuwa na thamani kwenye vinywa vya mashabiki wengi kama yalivyo madini yenyewe. 
Hata hivyo pamoja na Nataka Kulewa kumletea shida hivi karibuni kutokana na kutumia idea ya H.Baba mpaka watu kuanza kusema ameishiwa, mmoja ya wasanii wakubwa nchini anayesifika kwa kuufikisha muziki wa Bongo Flava hapa ulipo leo, bado ana imani kuwa Diamond si msanii wa kuchuja leo. Si mwingine ni Profesa Jay ambaye amesema Diamond ndio kama ameanza.
“Watu wanasema huu ndio mwisho wa @diamondplatnumz ,Dogo Ndio kwanza anafanya VEMA kama kuna sehemu anakosea si mngemrekebisha tu ili ASONGE?” ameandika Profesa kupitia Facebook leo.

Naye Nikki Mbishi wiki hii aliamua kutumia mtandao huo wa kijamii kumwaga sifa kibao kwa Diamond akidai kuwa ni msanii mwenye uandishi makini.
“Katika waimba bongo fleva,Diamond peke yake ndo anaandika kwa kuzingatia vina na mizani na baada ya yeye kufanukiwa wengine nao wanaweka vina kama Nai nai….changamoto daima,safi sana kuona kila mchezaji anacheza nafasi.”