SIZE 8 AONGOZA KWA KULIPWA FEDHA NYINGI ZAIDI AFRIKA MASHARIKI.....

SIZE 8 (4) (600x359) Website mbalimbali za nchini Kenya zimeandika kuwa Size 8 ndiye msanii wa kike wa Afrika Mashariki anayelipwa pesa nyingi zaidi.
Zimeandika kuwa kwa mujibu wa survey iliyofanywa hivi karibuni imebainika kuwa Size 8 ndiye msanii wa Afrika Mashariki anayepokea dau kubwa zaidi kwa show anazofanya na pia anatafutwa mno kwaajili ya kufanya shows.
Pamoja na show zingine, Size 8 amejipatia fedha nyingi kutoka kwenye kampeni za Niko Na Safaricom, Club 254 ya Airtel na Coca Cola.