"MAPENZI YAMENIPOTEZEA MUDA NA KUNIFANYA NUJUTE"....NISHA
STAA wa la filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amefunguka kuwa anajuta kupoteza muda mwingi kwenye mapenzi kuliko kazi mwaka jana.
Akiongea na mwandishi wetu, Nisha alisema amebaini kuwa mwaka 2012 mapenzi yalimfanya ashindwe kutimiza malengo yake mengi kwenye soko la filamu.
“Mwaka jana nilipelekwa puta sana na mapenzi. Mara kigogo, Geofrey na
Nay wa Mitego jambo ambalo lilinifanya nishindwe kufanya kazi kwa
ufanisi. Mwaka huu sikubali, mwendo wa kazi tu siyo mapenzi,” alisema
Nisha.
Aidha, aliongeza kuwa atahakikisha anashirikiana vizuri na wenzake katika kazi zake.