
Akizungumza kwa kujiamini hivi karibuni, Kadinda alisema yeye kama
meneja wa Wema, ana kila sababu ya kuongozana naye kila anapokwenda
kwani ndiye anayemchagulia nguo, viatu hadi ‘setting’ ya nywele.
“Watu wamesemasema sana juu ya safari yangu ya Sauzi na Wema…jamani mimi
ni kila kitu kwa Wema kwani ni meneja wake, napaswa kujua kila
anachokifanya, hata linapokuja suala la mavazi mimi ndiye
ninayemchagulia ‘so’ watu wasihoji sana,” alisema Kadinda.