SIJAPOTEZA MVUTO...BADO NALIPA"..SHAMSA FORD


DIVA wa filamu za Kibongo Shamsa Ford amefunguka kwamba, wanaosema eti amepoteza mvuto baada ya kujifungua wanakosea sana kwani ndiyo kwanza amezidi kuwa na mwonekano mzuri.

Akipiga stori na Mwandishi wetu jijini Dar es Salaam, Shamsa alisema: “Siamini kama kuzaa kunasababisha kupoteza mvuto lakini hata kama ndivyo basi kwa upande wangu hilo halijatokea. Ndiyo kwanza nimezidi kuwa na mvuto.”

Alienda mbali zaidi kwa kueleza kuwa kilichomsaidia zaidi kuongeza mvuto wake ni mazoezi na kuzingatia urembo.

“Asikudanganye mtu, hata kama hujazaa, mwanamke lazima azingatie masharti ya urembo na mazoezi ya mwili ili kuufanya mwonekano kuwa wa kuvutia, ndiyo maana unaniona hivi,” alisema Shamsa na kuongeza:

“Nadhani ndiyo sababu hata baba mtoto wangu (Dikson Matoke) ameongeza mapenzi kwangu, ni kwa sababu ya kujitunza,  amekuwa akiniambia waziwazi kuwa mvuto wangu kwa sasa ni mzuri zaidi.”