AFYA YA MATUMAINI YATENGAMAA
SHIRIKISHO la filamu nchini(TAFF) limesema, limefurahishwa na taarifa iliyotolewa na madaktari wa hospitali ya Amana kuwa afya ya msanii wa vichekesho Bi.Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’iposhwari na wamemruhusu kurudi nyumbani.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Rais wa Shirikisho hilo la filamu nchini(TAFF) Simon Mwakifamba alisema kuwa wao kama shirikisho wamepokea kwa furaha taarifa hiyo.
"Tunajisikia poa kwa afya ya msanii huyo kurejea kuwa nzuri, baada ya kuwa ameruhusiwa na madaktariwa hospitali hiyo ya Amana kwa kuwa amerudi nyumbani kwao Kiwalani jijini Dar es Salaam,"alisema Mwakifamba.
Afya ya msanii huyo ilibadilika na alianza kuumwa alipokuwa ameenda nchini Msumbiji na alipokelewa na wasanii wenzake kibao baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl.Julius Nyerere jijini Dar akiwa hoi kutokana na kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.