TRAFIKI AGONGWA NA GALI NA KUFA PAPO HAPO-DAR



Trafiki wa kike aliyejulikana kwa jina moja la Elikiza aliyekuwa akiongoza magari eneo la Bamaga, Mwenge jijini Dar, akifunikwa na wasamaria wema baada ya kugongwa na gari na inadhaniwa kuwa amekufa papo hapo.


Baadhi ya wananchi waliofika eneo la tukio.
Hali ilivyokuwa eneo la tukio baada ya ajali hiyo.

Trafiki mmoja ambaye amefahamika kwa jina moja la Elikiza, muda huu amegongwa na gari aina ya VX ambayo haikujulikana namba na inadhaniwa kuwa amekufa papo hapo wakati akiongoza magari eneo la mataa ya Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Taarifa zilizopatikana eneo la tukio zinadai kuwa Trafiki huyo alikuwa akiongoza msafara na baada ya msafara huo, aliruhusu magari mengine yaendelee na safari ndipo ghafla gari lilipotoka upande wa pili na kumgonga.

(Picha na Shauri Kati / GPL)