Waziri
wa Maliasili na Utalii,Mh. Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na
viongozi wa WMA ya Ikona wadau wa sekta ya utalii katika wilaya ya
Serengeti mkoani Mara
Maafisa wa Jeshi la Polisi Wilayani Serengeti wakiwa katika mkutano huo.
SERIKALI
imesema haitasita kuchukua hatua za kuzifunga kambi zote za kitalii
ambazo zimo katika maeneo ya Jumuiya ya Hifadhi za Wanyama pori
WMA,ambazo zitaendelea kukiuka sheria na Kanuni kwa kulipa mapato
yatokanayo na shughuli ya utalii kwa uongozi wa vijiji badala ya malipo
hayo kufanyika kupitia WMA.
Agizo
hilo limetolewa na waziri wa Maliasili na Utalii Mh Balozi Khamis
Kagasheki,wakati akizungumza na viongozi wa WMA ya Ikona wadau wa sekta
ya utalii katika wilaya ya Serengeti mkoani Mara.
Amesema
hivi sasa kumeibuka migogoro kwa baadhi ya WMA kwa kuhusisha viongozi
na wananchi wa vijiji husika ambayo imekuwa ikihatarisha amani na
mahusiano kati ya kijiji na kijiji kwa kugombea mapato baada ya baadhi
ya kambi za utalii kukiuka kanuni na kwa kulipa tozo hizo moja kwa moja
kwa baadhi ya serikali za vijiji kinyume cha sheria.
Waziri
Kagasheki,alifikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa mgogoro ambao
umekuwa ukiendelea katika WMA ya Ikona wilayani Serengeti umechangiwa na
baadhi ya kambi za kitalii kulipa mapato yake kwa baadhi ya vijiji
wakati wakitambua wazi kuwa kambi hizo ziko ndani ya eneo la WMA.
Kwa
upande wao baadhi ya wananchi na viongozi wa vijiji vitano vinavyounda
WMA ya Ikona,walimesema mgogoro huo pia umechangiwa na uongozi wa WMA
kushindwa kusoma taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi,madiwani
kujineemesha huku wananchi wakishindwa kuvuna mazao mashambani baada ya
kushambuliwa na wanyamapori kutokana tu na kuthamini shughuli za
uhifadhi.
WMA
ya Ikona inaundwa na vijiji vya Nyatambiso,Park
Nyigoti,Nyichoka,Makunduzi na Rubanda ambapo tayari WMA 38 zimeanzishwa
nchini 17 zikiwa zimetangazwa rasmi katika gazeti la serikali lengo
likiwa kuhakikisha wananchi wanahifadhi na kunufaika na raslimali hiyo
kwaajili ya kupunguza umasikini miongoni mwao.