Balotelii akilia kwa uchungu Mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli jana amejikuta akilia kama mtoto mdogo baada ya Spain kuifanya kitu mbaya Italia. Mbaya zaidi baada ya Spain kuinyuka Italia bao 4 kwa ‘nunge’ na kunyakua
kombe la Euro 2012, Balotelli alijikuta akikwaruzana na members wengine
wa timu yake ya taifa ya Italia.Baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa mjini Kiev na kuashiria kuwa
Italia hawana chao, mshambuliaji huyo wa Manchester City ya Uingereza
alijikuta akibishana na viongozi wa juu wa timu hiyo kwenye chumba cha
kubadilishia nguo na inasemekana alimsukuma mmoja.Baada ya dakika kadhaa, Balotelli alionekana tena uwanjani kwenda
kupokea medali yake lakini alijikuta akitokwa na machozi ya uchungu na
kushindwa kujizuia na hali hiyo.Hata hivyo kocha wa Italia, Cesare Prandelli amesema Balotelli ataizoea tu hali hiyo iliyomuumiza sana.‘Niimwambia Mario kwamba haya ni mambo ambayo inabidi ukabiliane nayo na
uyakubali,” alisema Prandelli. ‘Inabidi mshikane mkono na uwaambie
wapinzani wako kuwa ni wazuri, kubali kushindwa.”‘Lakini inabidi kuhakikisha kuwa hili linakusaidia kusonga mbele na
kukua kutokana na matokeo hayo. Hili limetokea kwa wachezaji wengi, na
litatokea tena, lakini hivi ndivyo mchezo ulivyo.’