BARUA YA ZITTO KABWE INAYOMTAKA "LWAKATARE ATIMULIWE CHADEMA" YAZUA BALAA


CHADEMA taifa vipande vipande! Soma barua hii ya Zitto 

zitto kabwe ameandika barua kwa katibu mkuu dr slaa akitaka mambo mawili yafanyike ..


1.Lwakatare achunguzwe na chama 
2.Lwakatare ajiuzulu nyadhifa zote alizokuwa nazo ndani ya chama 
3. Ushauri huu usipofanyiwa kazi atafanya maamuzi magumu yatayokigharimu chama zaidi.

Taarifa zaidi kutoka ndani ya vyanzo zinaeleza kuwa kitilla mkumbo naye ameandika barua kama ya zitto lakini yeye anataka lwakatare atoswe kwa sababu ameshachafuka ili kukinusuru chama...

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa ushauri huu umesababisha mtafaruku na mgawanyiko mkubwa ndani ya uongozi wa taifa kwani baadhi wanapinga ushauri na wengine wanaunga mkono.
Wanaopinga wanadai kuwa lwakatare alikuwa kazini hivyo lazima chama kimlinde hadi dakika ya mwisho..
Hata hivyo,Leo Zitto Kabwe amezijibu tuhuma za barua hii akiadai kushangazwa jinsi barua hii ilivyovuja na kuishia kusema kuwa kuna kirusi ndani ya chama chao
Source:Jamii Forums