Wakati
mwingne wanaume au watu tofauti hudhani kwamba, wanawake wanaovaa nusu
uchi huwa wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa wanaume.
Inawezekana kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini wapo wale
ambao wanalipa fidia kutokana na kuamini kwao kwamba wanamapungufu kwa
mfano sura zao zimewaangusha, hivyo miguu yao mizuri inabidi kuziba
pengo au udhaifu huo.
Wakati mwingine hata wanawake wanaodhani au
kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa wakivaa nguo fupi zinazoonyesha
maungo yao.Hawa nao ni
lazima wanalipa fidia ya kasoro fulani waliyo nayo.
Inawezekana
wameshindwa kulinda ndoa zao, au inawezekana hawajaolewa na sasa
wanataka kuonyesha kwamba, pamoja na kutoolewa kwao, bado wao wana sura
na miguu au miili mizuri.
Udhaifu wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au kupitia nyuma ya ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo kuyatangaza yale maeneo ya mwili wake ambayo anaamini ni mazuri.
Udhaifu wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au kupitia nyuma ya ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo kuyatangaza yale maeneo ya mwili wake ambayo anaamini ni mazuri.
Kuyatangaza huko
humpa ahueni kwa kuamini kwamba bado anayo thamani, kwani ataangaliwa
sana na wanaume, kusifiwa na pengine kutongozwa.
Hebu angalia wanawake ambao wanavaa nguo za kubana huku wakiwa na makalio makubwa. Hawa mara nyingi wana sura ambazo wao au wengi huamini kwamba ni mbaya.
Hebu angalia wanawake ambao wanavaa nguo za kubana huku wakiwa na makalio makubwa. Hawa mara nyingi wana sura ambazo wao au wengi huamini kwamba ni mbaya.
Huvaa nguo hizi ili kuonyesha kwamba, pamoja na ubaya wa sura
zao, bado wao ni wazuri sana katika maeneo mengine ya mwili ambayo
wanaume na hata wanawake wengi huyapenda au kutamani kuwa nayo.
Wengi hawavai tu nguo hizi za kubana kwa sababu ni fasheni, la hasha, wengi hili ni kimbilio la udhaifu wao