Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amewatuliza Watanzania kuhusu kupanda kwa nauli akisema ameyapokea malalamiko yao na atayafanyia kazi.
Kwa kuanzia ameagiza nauli za treni jijini Dar es Salaam zisipande
bali ziendelee kutozwa za zamani mpaka taarifa zaidi itakapotolewa.
Mwakyembe alitoa kauli hiyo alipozungumza kwenye Bonanza la Vyombo vya Habari lililofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Alisema ni kweli Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(Sumatra|) ilitangaza nauli mpya, lakini kwa kilio cha Watanzania
ataangalia sababu za kupandisha huku akishirikiana na wasafirishaji
kujua ukweli.