SNURA, BONITHA watwangana, chanzo eti ni Wema

MUIGIZAJI wa ‘long time’ Snura Mushi na demu mmoja wa mjini  anayetambulika kwa jina la Bonitha,
juzi kati walitwangana ngumi kwa kile kinachodaiwa kuwa kila mmoja anataka awe karibu na Wema Sepetu.
Tukio hilo lilitokea maeneo ya Mwananyamala Komakoma, Dar Aprili 2, mwaka huu katika saluni ya Bonitha ambapo Snura alifika hapo akiwa ameongozana na Wema pamoja na Mtangazaji wa Kipindi cha Friday Night, Lady Nah kinachorushwa na Runinga ya EATV ya jijini Dar.
Akizungumza na Ijumaa baada ya kutokea vurugu hizo, Bonitha alisema kuwa hakuelewa kilichotokea hadi Snura kwenda kumfanyia fujo ndani ya ofisi yake zilizosababisha watwangane.
Sinura alipoulizwa kuhusu ishu hiyo alisema:
“Kiukweli nimechoshwa na maneno anayonitangazia Bonitha, mara aseme mimi bwana wangu ni (anataja jina la kigogo maarufu Bongo) na maneno mengine ambayo hata kuyatamka naona aibu lakini kikubwa ni baada ya mimi kuwa karibu na Wema, hicho ndicho kinachomuuma anahisi kuna vitu nafaidi kumbe mi’ niko naye kwa ajili ya kurekodi filamu yake,” alisema Snura.
Baada ya kutokea fujo hizo Bonitha alienda kufungua kesi katika Kituo cha Polisi cha Garden na kupewa RB yenye namba Gar/RB/384/2012 SHAMBULIO NA KUHARIBU MALI.