Pato lake lapungua kwa asilimia
40
Lakini bado anatengeneza pauni
Milioni 29 kwa mwaka.MWANASOKA nyota, David Beckham amepunguziwa mshahara kwa
zaidi ya dola za Kimarekani Milioni mbili — ambayo ni sawa na kushuka kwa
asilimia 40 ya pato lake.
Inamaanisha nyota huyo wa LA Galaxy ameondoka kwenye orodha ya wanasoka wanaolipwa fedha nyingi katika Ligi ya Marekani, akina Thierry Henry, ambaye anachezea New York Red Bulls.
Becks, mwenye umri wa miaka 37,
amekuwa akilipwa zaidi ya pauni Milioni 4 (dola Milioni 6.5) kwa mwaka.Lakini
amekubali kulipwa pauni Milioni 2.5, baada ya kuamua kubaki California na mkewe
Victoria, mwenye umri wa miaka 38, na watoto wao wanne.Inamaanisha nyota huyo wa LA Galaxy ameondoka kwenye orodha ya wanasoka wanaolipwa fedha nyingi katika Ligi ya Marekani, akina Thierry Henry, ambaye anachezea New York Red Bulls.
Pamoja na hayo, anapata makato ya
mauzo ya tiketi za Galaxy na vifaa vya michezo. Na ataendelea kupata kiasi cha
jumla ya pauni Milioni 29 kwa mwaka, kupitia dili za mauzo ya nguo na maslahi ya kibiashara, ( jarida la
Forbes.)Nahodha huyo wa zamani wa England, Becks angeweza kujiingizia fedha
nyingi zaidi kama angekubali kuhamia Paris Saint-Germain.