JUMA KASEJA BADO ANA UCHUNGU NA MAFISANGO. JANA JIONI ALISHINDWA KUJIZUIA NA KUJIKUTA AKIMWAGA MACHOZI HADHARANI KATIKA SHOW YA SIMBA DAR LIVE.


KIPA wa Simba, Juma Kaseja jioni hii ameshindwa kujizuia lilipotajwa jina la Patrick Mafisango kwenye sherehe za ubingwa wa Ligi Kuu ya klabu hiyo na kujikuta akimwaga machozi kwenye ukumbi wa Dar Live, Mbagala, Dar es Salaam.

Kaseja alimwaga machozi wakati alipokuwa akipokea Medali kwa niaba ya marehemu Mafisango aliyefariki dunia wiki iliyopita kwa ajali ya gari maeneo ya Keko, Dar es Salaam ambapo alizikwa kwao DRC siku tatu baadae.
Kiungo wa Simba, Salum Machaku aliitoa Medali aliyokabidhiwa kwenye sherehe hizo kwa marehemu Mafisango ambapo Kaseja alinyamaza baada ya kubembelezwa na wachezaji wenzake na kuendelea na shughuli hiyo iliyofana na kuhudhuriwa na mamia ya wapenzi wa klabu hiyo.



Ukumbi pamoja na mapambo yaliyowekwa,  ulipendeza zaidi kwa mavazi ya mashabiki wa Simba ya rangi nyekundu na nyeupe ambapo Meneja wa Global Publishers Limited, Abdallah Mrisho alikabidhi Sh. Milioni 3 kwa Kaseja kama zawadi yao kwa Simba kutokana na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.
Baada ya yote hayo, wachezaji na viongozi wa Simba walifungua shampeni na sherehe ikaanza rasmi, bendi ya Msongo Ngoma ikianza kutumbuiza, ikiongozwa na mwimbaji wake mkongwe, shabiki maarufu wa Simba, Mzee Muhiddin Mwalimu Gurumo.   (Stori imeandikwa na Bin Zubery )



Amos Makalla Mbunge wa Jimbo la Mvomero,akimkabidhi medali Juma Kaseja nahodha wa Simba.
Kaseja akilia kumpoteza Mafisango.