Mdada wa kazi aliyesababisha kifo cha mtoto akamatwa


Mdada huyo aliyekuwa akifanya kazi za ndani hapa Dar es salaam maeneo ya Sinza mapema mwezi huu alisababisha kifo cha mtoto wa mwajiri wake mwenye umri wa miezi 8.Dada huyo baada ya kusababisha kifo alimuacha mtoto akamlaza kitandani kama amelala na yeye kutokomea
kusikojulikana.Baada ya kufanyiwa vipimo mtoto alionekana amekufa baada ya kuzibwa pumzi.
Mdada huyo baada ya kukimbia akawa yupo hapa hapa Dar akapata na bwana akawa anaishi nae.Kama bahati mmoja wa vijana anaemfahamu wakati akifanya kazi kule alipofanya tukio akamuona.Baada ya kumfatilia akajua anapoishi na ndipo alipokuja kukamatiwa.

Baadae alikuja kubebwa na polisi kwenye hilo defender,habari zaidi sikiliza leo tena katika heka heka za leo.
CHANZO Dina Marious na kipindi cha leo tena cloud