Miss Jokate



Upepo wa habari za chini ya kapeti umemgeukia Miss Jokate Mwegelo, mrembo namba 2 kwenye Shindano la Miss Tanzania 2006, nyuma ya mshindi Wema Sepetu aliyevaa taji kuwa msichana huyo havumi lakini yumo kwenye msafara wa matukio ya kimapenzi.

Mitandao mingi ya kijamii hivi karibuni imemfumua Jokate kuwa ni simba mwenda kimya mawindoni kufuatia msanii wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul ‘Diamond’ kuutangazia umma kuwa anatoka na mrembo huyo.

Siku chache zilizopita, Wema Sepetu ambaye alikuwa mchumba wa Diamond kabla hajabwaga manyanga alilalama kwenye vyombo vya habari kuwa Jokate ameingilia penzi lake kwa msanii huyo, tuhuma ambazo miss huyo namba 2 aliziruka kwa kusema anasingiziwa.
“Si alikuwa anakanusha, sasa yako wapi?” Jane Swai, mchangiaji wa blogu (jina kapuni) alihoji wakati akitoa maoni yake kuhusu habari ya Diamond kutangaza rasmi kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na msichana huyo mwenye kidoti cheusi usoni na kwamba haoni mwingine wa kumpa penzi lake.

Wakati Jokate akisakamwa kwenye mitandao, Uswahilini nako hali si shwari ambapo dodoso nyingi zisizokuwa na uthibitisho wa kutosha zimekuwa zikitolewa kwamba mwanadada huyo kabla ‘kudeti’ na Diamond ameshatoka na msururu wa wanaume wengine.
Wachache kati ya wanaume wanaotajwa mitaani na ambao Jokate amekuwa akikanusha vikali kutoka nao kama alivyokuwa akikana kwa Diamond ni Hashim Thabeet, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ na Ambwene Yesaya ‘AY.’

“Jokate ni msiri lakini ameshatoka na (anawataja mastaa hao waliopo  paragrafu ya juu) na hata …(anamtaja kijana mmoja ambaye baba yake ana wadhifa mkubwa serikalini) naye ametembea naye, hata mzee… (anamtaja mfanyabiashara maarufu nchini) ameshapita, ni vema awe wazi kuna siku ataumbuka,” alidai Julieth John, mwanamitindo anayefanya shughuli zake jijini Dar es Salaam.
Siku chache tangu Diamond aanike kile kilichokuwa kikifichwa kati yake na miss huyo namba 2, mchumba wake wa zamani, Wema alitoa kauli hii: “Niliposema watu waliniona mjinga lakini sasa Jokate kaumbuka.”
 Jokate kwa upande wake amekuwa kimya.