OFFICIAL VIDEO: SHETTA ft DIAMOND - NIDANGANYE






Mapenzi ni uongo??Ni swali gumu ambalo laweza kuwa jepesi pia!Usishangae na wala usibishe.Ndio ukweli.Kinyume cha hapo unaniongopea.Nidanganye. Kuna wakati lala lalal lalala za mapenzi hujaa uongo unaopendeza. Wenzetu wa huko mbele wanasema Sweet Nothings.Utupu. Ukweli unauma…nakupenda!
Kuna wakati mapenzi hupumbaza.Unachoambiwa na mhusika ndicho unachokielewa na kukikubali. Nakupenda wewe zaidi ya mwingine.Unakubali hata kama kila mtu anakwambia sio kweli.Mpo wengi. Analosema ndio sheria.Ni wewe tu.

Maudhui hayo ya mapenzi ndio yaliyomo katika wimbo mpya kutoka kwa Shetta akiwa amemshirikisha Diamond. Kama wimbo unavyoitwa Shetta na Diamond wanasema Nidanganye…ukiniambia ukweli roho itauma sana.Nitaumia. Diamond anasema kwenye chorus kwamba  hata akimkuta chumbani kakumbatiwa…mmmmh!!
Hii ni production nyingine kutoka kwa KGT. KGT ni Producer ambaye kwa maoni yangu,he is one of the best. Hasikiki sana kama wengine coz he is such a cool and quite guy. Huu hapa Nidanganye.

<<DOWNLOADF HERE>> (Shetta_ft_Diamond_-_Nidanganye.mp3)
VIDEO YAKE NDO HII