‘Uwoya ananivunjia ndoa’

 

Chokochoko zimeanza! Mwanadada anayepatikana kwenye tasnia ya Bongo Movies, Janet Mathias amedai kuwa Irene Uwoya anataka kumvunjia ndoa, Risasi Jumamosi lina kitu na boksi.
KABLA YA MADAI

Habari za awali zilidai kuwa Janet aliyekuwa shosti mkubwa wa Uwoya alianza mtafutano na staa huyo pale alipotajwa kumpindua kwa mumewe Hamad Ndikumana ‘Kataut’ mwishoni mwa mwaka jana.
Kuna habari za mjini kuwa, Janet na Uwoya ambao walifahamiana kitambo wakiwa wasichana wabichi, wamekuwa wakitibuana mara kwa mara hasa wanapozidiana ujanja katika mambo yao ya wanaume.

HUYU HAPA JANET
Akilia kuchezewa rafu mbele ya Risasi Jumamosi katikati ya wiki hii, Janet alisema kitendo cha Uwoya kumtangaza kuwa alitembea na mumewe kilimhatarishia ndoa yake mbichi aliyofunga miaka miwili iliyopita na mwanaume aliyemtaja kwa jina moja la Blaise.
“Unajua mimi ni mke wa mtu tena ndoa yangu ni mbichi, Irene anaponitangazia kuwa natembea na Hamad unafikiri anataka nini kama si kunivunjia ndoa yangu?
“Ukweli ni kwamba kila mume wangu anaposikia hizi habari huwa naponea kwenye tundu la sindano kuachika.
“Nimeshaambiwa kuwa ameapa kuvunja ndoa yangu kwa sababu anaona ndoa yake ilimshinda sasa anatangatanga,” alisema Janet ambaye ameuza ‘nyago’ katika filamu ya Vita Baridi na Last Card.

UWOYA AJIBU MAPIGO
“Ni kweli Janet alikuwa rafiki yangu sana, lakini kuna sababu kuu tatu zimenifanya niachane naye.
“Ni muongo, mgombanishi na kubwa kuliko nilipogundua kuwa anakula unga nikaona nikae pembeni, siifikirii ndoa yake.”
CHANZO Global publisher :NEWS