Askofu Malasusa: Wanasiasa Msiteke Nyara Mchakato Wa Katiba


Pamela Chilongola na Bakari Kiango.

WANASIASA nchini, wametakiwa kuacha kujihusishana suala la katiba na badala yake, suala hilo liachwe mikononi mwa wananchi.Rai hiyo ilitolewa jana na jijini Dar es Salaam na Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ,Askofu Dk Alex Malasusa, alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa Usharika wa Kinyerezi.
Dk Malasusa alisema katiba ya nchi si mali ya wanasiasa wanaotaka kuiteka nyara na kwamba hiyo ni mali ya Watanzania, wanaopaswa kupewa uhuru wa kujadili kwa kina.
Dk Malasusa alisema wananchi wanapaswa kuwa na fursa kubwa ya kuboresha mchakato wa kuandika katiba hiyo, lakini wanakwamishwa na asilimia kubwa ya wanasiasa, wanachangia.

“Sina ugomvi na wanasiasa katika suala hili, ila naomba wawaachie wananchi, kwanza ili wapate fursa ya kuchangia maoni yao,” alisema Dk Malasusa.Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuchangia maoni yao ili kuboresha katiba inayotarajiwa kuandikwa kwa manufaa ya wananchi wote.

“Wote mjitokeze na kutoa maoni yenu, msikae kimya katika mchakato huu, alisema Dk Malasusa.Pia aliwataka waumini wa kanisa hilo, kubadilika na kufanya mambo yasiyomchukiza Mungu.Alisema lengi la kanisa hilo ni kujaribu kuwasaidia waumini wake, ili waweze kubadilika na si vinginevyo.