EXCLUSIVE: MATOLA NJIANI KUWA KOCHA MPYA WA AFRICAN LYON

Rahim Zamunda akiwa na mmiliki wa klabu ya Portsmouth Suleiman Al-Fahim
Klabu ya African Lyon imemtimua kazi kocha wake Jumanne Chale, baada ya timu hiyo kufanya vibaya kwenye ligi kuu ya Tanzania bara msimu uliopita.

Kwa mujibu wa mmiliki wa klabu hiyo Rahim Zamunda amesema kwamba wamefikia uamuzi huo ili kuweza kuisuka upya vizuri timu yao itakayoweza kupambana vizuri na mashindano yajayo.
"Huu ni uamuzi tuliofikia ili kuweza kuleta mabadiliko chanya kwenye timu yetu, na kwa sasa tupo kwenye mazungumzo ya mchezaji wa zamani wa Simba, Selemen Matola ili aweze kuwa bosi wa benchi letu la ufundi. Mpaka sasa tumefikia pazuri na lolote linaweza kutokea,"