LADY JAYDEE KUTEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA JUNE 30. UNGEPENDA KUUNGANA NAYE?

Mwanamuziki mkongwe nchini, Judith Wambura maarufu Lady Jaydee amepanga kukitembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre kilichopo jijini Dar es Salaam jumamosi ya June 30.

Katika ziara hiyo,mwanadada huyo atakula chakula cha mchana na yatima hao na kuwapelekea misaada mbalimbali.
Jaydee atakayeongozana na watu wake wa karibu ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kituo hicho kumwandikia barua tarehe 30 mwezi uliopita kumuomba afanye hivyo.
“Mheshimiwa, Rejea kichwa cha habari hapo juu. Maunga Centre ni kituo cha kulea watoto yatima.


Kituo kipo Kinondoni Mkwajuni mkabala na kituo cha Police Hananasif. Kituo kina watoto 50 kati yao 27 wanaume 23 wanawake.

Madhumuni ya barua hii ni kukuomba kuwatembelea watoto hawa yatima ambao wamepoteza wazazi wao.
Tunakuomba wewe pamoja na marafiki zako, ndugu na jamaa, wadau, wafanyakazi wako waje kupata baraka za Mungu ili wapate mafanikio katika shughuli zao za kila siku.

Kumbuka kuwatembelea yatima, kuwasaidia,kuwafariji kwa kuondokewa na wazazi wao ni ibada kubwa kwa dini zote kwani suala la yatima halichagui dini wala kabila.
Tunaamini kwa kufanya hivyo Mungu atakujaalia atakuzidishia kipato.

Tunakuomba siku yoyote utakayokuwa na nafasi na sisi tunapendekeza iwe mwanzoni mwa mwezi huu wa sita.
Tunaamini kwa jambo hili la kijamii tutapata majibu mazuri na muafaka. Mwenyezi Mungu ametuagiza kuwafariji yatima na hakuna suala Mungu aliloweka kipaumbele kwa dini zote kama hawa yatima.

Jukumu la kuwatunza yatima ni la kwetu sote. Tunakuombea kwa Mungu akupe Roho ya Imani na kuweza kurupa majibu mazuri
Tunatanguliza Shukrani za awali.
Lady Jaydee pia ametawaka watu wengine watakaopenda kuchangia chochote wawasiliane naye kwa e-mail: judyjaydee@yahoo.com ama kupiga simu moja kwa moja kwenye kituo hicho kwa namba 0714-607999 au 0652-385046.

Hongera Jaydee kwa kuwa na moyo wa kuisaidia jamii.