KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia na Mbunge Bumbuli, January Makamba (katikati) na Mbunge wa Singida, Mohamed Dewji (kulia) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Simanjiro,Christopher Ole Sendeka (kushoto) na Mbunge wa Viti Maalum Ester Bulaya kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dkt. Makongoro Mahanga(kushoto) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige wakati wa mapumziko ya mchana ya Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma.
Baadhi ya wabunge wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakijaza fomu za vitambulisho vya Taifa leo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda (katikati) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Simanjiro,Christopher Ole Sendeka (kushoto) na MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (kulia),wakati wa mapumziko ya mchana ya kikao cha Bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda(kulia) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Simanjiro,Christopher Ole Sendeka (kushoto) wakati wa mapumziko ya mchana ya kikao cha Bunge bajeti linaloendelea mjini Dodoma.
Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi (SUGU) akibadilishana mawazo na Mbunge Mwenzie kutoka Jimbo la Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe wakati wa mapumziko ya mchana ya Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu/Tiganya Vincent- MAELEZO-Dodoma.