LINAH AFUNIKA IRINGA

 Msanii wa kizazi kipya Linah Jumamosi June 10, 2012  akiwa V.I.P. Club Iringa alifanya show ya kukata na shoka katika mashindano ya kumtafuta mlimbwende wa REDDS Miss Iringa iliyojaza mashabiki kutoka kila kona, picha juu na chini Linah akijiweka tayari kabla hajapanda kwenye jukwaa.
 Picha juu na chini Linah akijikagua kama kila kitu kipo sawa 
 Msanii wa kizazi kipya Linah akipata Ukodak moment na mashabiki katika mashindano ya kutafuta Mrembo wa REDDS Miss Iringa
 Linah katika pozi na mmoja ya shabiki.
 Mtu nyomi wakiwa V.I.P. Club jijini Iringa.
 Shabiki akiteremka toka jukwaani baada ya kumtuza Linah
 Linah akifanya vitu vyake,
Linah akiendelea kupagawisha mashabiki.