MISS TANZANIA - DEMU WA KANUMBA ANAOLEWA



MMOJA wa wasichana waliojitangaza na kukiri kuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa marehemu Steven Kanumba, Husna Maulid, ambaye alikuwa Miss Kinondoni namba 2 na kupata tiketi ya kushiriki Miss Tanzania japo hakufanya vizuri sana,  anaolewa.
Husna ambaye hivi karibuni ameanza  kuigiza akiwa mmoja ya washiriki wa series ya 69 Records, ameripotiwa kuchumbiwa na kwamba ndoa inafuata muda si mrefu.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Husna anatarajiwa kuolewa na 
Abubakar Jumbe
"Huwezi aamini wiki ijayo Husna atakuwa mke wa mtu, mipango yote imeshafanyika na mahali imeshatolewa.".....
 Mtandao huu uliasiliana na Husna mwenye na alikuwa  na haya ya  kuongea: "Ni kweli nimechumbiwa na wiki ijayo Ijumaa naolewa.Mume wangu mtarajiwa anaitwa Abubakar Jumbe." - Husna.