Redefine Possible: Mcanada asiye na miguu akwea Mlima Kilimanjaro


Mapema wiki hii Spencer West, raia wa nchini Canada, 31, asiye na miguu ameukwea mlima mrefu kuliko yote barani Afrika, Mt. Kilimanjaro kwa kutumia mikono.
Akiwa na wheelchair, marafiki alioongozana nayo pamoja na uvumilivu, West amethibitisha kuwa hakuna linaloshindikana.
Safari hiyo ilimchukua siku saba mpaka kufika kileleni mwa mlima huo ulio fahari ya Tanzania.
West, mwenye urefu wa futi mbili na inchi saba alitumia asilimia 80 ya safari yake kuukwea mlima huyo wenye urefu wa metre 5,895 kwa kujivuta na mikono yake.
Alijiandaa na safari hiyo kwa msaada wa ‘personal trainer’, lakini alikubali kwenye mahojiano na CTV News kuwa safari hiyo ilikuwa ngumu kuliko alivyokuwa anafikiria.
“Mpaka nafika kileleni mikono yangu ilikuwa haijiwezi, mabega yangu yalikuwa yamevimba lakini kuna kitu cha kuzungumzwa kuhusu kujituma na kujaribu kufikia malengo,” West alielezea kwenye interview na CTV.
Ni kwa kupitia habari kama hizi ambapo tunakumbuka kuwa kila kitu kinawezekana pindi unapoiweka akili kwenye jambo fulani. Ama kweli West ametoa tafsiri mpya ya ‘uwezekano’.
 by Wordpress