COCA COLA YASIKITISHA MKATABA NA RONALDINHO BAADA YA KUONEKANA NA VIKOPO VYA PEPSI.

Ronaldinho akiwa katika mkutano na waandishi wa habari huku mbele yake akiwa na vikopo vya pepsi ambavyo vilipelekea Coca Cola kusitisha mkataba naye.



 KIUNGO nyota wa kimataifa wa Brazil, Ronaldinho Gaucho ameendelea kukumbwa na matukio baada ya kampuni ya Coca Cola kusitisha mkataba na mchezaji huyo ambaye kwasasa anakipiga katika klabu yake mpya ya Atletico Mineiro. Ukiwa umepita mwezi mmoja toka alipoondoka katika klabu ya Flamengo kutokana na klabu hiyo kushindwa kumlipa mshahara wake, Ronaldinho anatuhumiwa kukiuka makubaliano ya mkataba na Coca Cola ambapo toka amesaini mkataba huo hata mwaka haujatimiza. Mkataba huo mnono unaofikia kiasi cha dola 737,400 kwa mwaka ambao ungeisha wakati wa Kombe la Dunia 2014 litakalofanyika nchini humo ulikatishwa kutokana na Ronaldinho kuonekana akiwa na mkopo ya pepsi wakati wa mkutano wa waandishi wa habari. Kampuni ya Pepsi ndiyo wadhamini wa klabu ya Atletico Mineiro hivyo makopo ya kampuni hiyo kuonekana katika mkutano wa waandishi wa habari sio uamuzi wa Ronaldinho hata kama aliwahi kuwa na mkataba na kampuni ya pepsi zamani kabla ya kusaini mkataba na Coca Cola. Lakini chanzo hicho kinaonekana sio pekee kilichopelekea Coca Cola kusitisha mkataba huo , kutokana na matukio mbalimbali ya vituko vya mchezaji huyo haswa baada ya Flamengo kutoa mkanda wa video ukimuonyesha mchezaji akiingia na vimwana katika hoteli ambayo timu hiyo ilikuwa imeweka kambi. Mbali na tukio hilo pia kuna picha zilizopigwa katika kompyuta zikimuonyesha mchezaji huyo akijichua Novemba mwaka jana.