Mtoto wa kambo wa Usher bado mahututi kwa kugongwa na boti


Mke wa zamani wa Usher, Tameka Foster amezungumza (exclusively) na mtandao wa RadarOnline.com baada ya mtoto wake Kyle mwenye miaka 11 kugongwa juzi na boti (jet ski) mjini Atlanta.

“He’s bad,” aliuambia mtandao huo kuhusu mwanae wa kiume aliyempata kwenye ndoa yake yake na Ryan Glover.
Kyle aligongwa na jet ski iliyokuwa ikiendeshwa na mwanaume mwenye miaka 38 wakati mtoto huyo alipokuwa akicheza kwenye tube iliyokuwa ikivutwa na boti akiwa na mtoto mwingine kwenye ziwa Lanier.
Usher ana watoto wawili na Tameka; Usher V, miaka mine na Naviyd, miaka mitatu.
Licha ya wanandoa hao wa zamani kuwa kwenye mzozano mkubwa mahakamani wa kugawana watoto, Usher ameendelea kuwa karibu na watoto wengine watatu wa Tameka na amekuwa akiwasaidia kwa namna yoyote awezayo.
Mtandao wa E! Online uliripoti kuwa Usher alikodi ndege ili kumchukua Tameka aendee kumuuguza mwanae aliyelazwa kwenye hospitali ya watoto ya Egelston jijini Atlanta.
“Kyle, You are strong.. You’ll be saved I know it. I love you my baby. I need all #Prayers for my son! thanks you everybody!” Aliandika Tameka kwenye ukurasa wake wa Facebook.