MWALIMU ACHAPWA VIBAO NA WANAFUNZI BAADA YA KUTOSHIRIKI MGOMO


MWALIMU  mmoja  wa jinsia ya kike aliyefahamika kwa jina moja  la Kahimba  wa shule ya msingi  ya Kambarage  iliyopo    Kata ya Msamala katika Halmashauri ya  Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma  amajeruhiwa vibaya  kwa kupigwa  sehemu mbalimbali za mwili  na kundi  linalodaijwa kuwa ni la wanafunzi wa shule hiyo ambao  wanadaiwa kuwa na hasira  baada  ya walimu wengi wa shule hiyo kutoonekana  eneo la shule kufuatia mgomo wa chama cha Walimu  (CWT).

Akizungumuza na waandishi wa habari hizi Mjini Songea  mwalimu mkuu wa shule ya msingi  Kambarage  Adolfina Ndunguru alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alidai kuwa  ni udhalilishaji  mkubwa kwa mwalimu kupigwa na wanafunzi.

Ndunguru alisema kuwa  yeye pamoja na walimu wenzake hawakuweza kufika  kwenye eneo la shule kwa kuwa wao ni walimu ambao wamekubaliana kugoma  kutokana na Serikali  kushindwa kutimiza  ahadi yao wanayodai.

Alifafanunua kuwa  inadaiwa kundi la wanafunzi lilipomuona mwalimu Kahimba kwenye  eneo la shule hiyo lilimvamia na kuanza kumpiga mawe sehemu  mbalimbali za mwili na baadaye  alifanikiwa kukimbia.

Kwa upande wa baadhi ya walimu  wa shule za msingi, Sekondari na Chuo cha Ualimu cha Songea kilichopo Manispaa ya Songea ambao wameomba majina yao yahifadhiwe walisema kuwa  mgomo utaendelea mpaka Serikali itakapo ridhia kuwalipa madai yao hasa ikizingatiwa kuwa  wao wanafanyakazi katika mazingira magumu.

Waandishi wa habari walifanikiwa kutembelea baadhi ya shule  za Msingi na sekondari ambazo zilikuwa hazina walimu kabisa na kwamba wanafunzi wa shule hizo  wakiwa wamezagaa mitaani huku wakiinung`unikia Serikali kwa kuto watendea haki walimu wao ambao alikuwa wakiwaandaa wanafunzi katika Mitihani  ya kumaliza Elimu ya Msingi na sekondari.

Shule zilizotembelewa na waandishi wa habari ambazo hazikuwa na walimu kabisa  ni Shule  za Msingi za Matarawe, Mwembechai, Sabasaba, Mkombozi, Kawawa, Mfaranyaki, Majengo, Songea, Kambarage, Msamala na Majimaji na shule za sekondari za matarawe, Mfaranyaki, Shule ya wavulana Songea na Shule ya wasichana  songea.

Kwa upande wake mmoja  wa wanafunzi  wa shule ya msingi Majimaji Tamimu Ajali anayesoma darasa la tano ameiomba Serikali kuharakisha kutekeleza madai ya walimu  wanayodai kwani bila kufanya hivyo kunauwezekano mkubwa  wa kushuka kwa kiwango cha Elimu hasa  ikizingatiwa kuwa  wanafunzi wapo kwenye maandalizi ya kufanya mitihani.

Tamimu alisema kuwa  ni vyema serikali ikatambua umuhimu  wa mwalimu kwa kumuuongezea mshahara  sawa na taaluma  zingine muhimu kwa mfano. Wanajeshi, Madaktari,Wauguzi na wahudumu wa afya.

Afisa Elimu wa halmashauri ya Manispaa ya Songea  Fulgensi Mponji amethibitisha kuwepo kwa mgomo huo wa walimu  amabapo alisema Manispaa hiyo ina shule  72, Sekondari za Serikari 23, Shule za seskondari za binafsi 13 ambazo  idadi kubwa ya walimu hawakuwepo kwenye maeneo yao ya kazi.

Alisema kuwa tayari ameshawaagiza walimu wakuu  wa shule za msingi na waratibu Elimu  kata wote kukutananao katika shule ya msingi Mfaranyaki  kwa lengo kuwakutanisha walimu ili kuzungumzia namna ya kutatua tatizo hilo.

Naye  Katibu wa chama cha walimu mkoa wa Ruvuma  Luya Ng`onyani alisema kuwa mgomo  huo ni halali na umezingatia sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu cha  80 (1) ambapo hatua ya kwanza CWT kwa niaba  ya wanachama tayari imetekeleza  kutangaza mgogoro wa siku 30 kwa kujaza fomu  CMA No: 1.

---
habari via dj-sek.blogspot.com


Wanafunzi wa shule za msingi Bwawani na Kijichi Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, wakiandamana jana Jumatatu Julai 30, 2012, kupinga haki yao ya msingi ya kupata elimu kuvurugwa kufuatia mgomo wa walimu ulioanza rasmi jana. Wanafunzi hao waliandamana umbali wa kilomite 10 hadi ofisi za Afisa elimu wa manispaa hiyo na kueleza "kesi" yao ambapo wameitaka serikali kumalizana na walimu ili wao wasome.
Wanafunzi wa shule za Makuburi na Mabibo, wakiwa chini ya mwembe, jana asubuhi Jumatatu Julai 30. Walimu wengi hawakuingia madarasani kufundisha jana wakiitikia mwitoi kutoka chama cha walkimu nchini kilichowataka kutofanya kazi leo Jumatatu na kuendelea hadi madai yao kuhusu maslahi yatakaposhughulikiwa na serikali.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Makuburi, wakijisomea baada ya walimu shuleni hapo kugoma kufundisha jana Julai 30, 2012. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, ambaye hata hivyo alikataa kutaja jina lake, alisema walimu walifika lakini hawakufanya kazi wakiunga mkono agizo la rais wa chama cha walimu Gratian Mukoba, aliyewataka walimu wote kushiriki mgomo usio na kikomo kuanzai leo Jumatatu.
Afisa Elimu Taaluma wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Juliana Mlay (Kushoto) akitafakari nini cha kuwaambia "Wageni" wake, wanafunzi wa shule za msingi Kijichi na Bwawani za jijini walioandamana umbali wa kilomita 10 hadi ofisini hapo wakilaani kutosoma jana, kufuatia mgomo wa walimu ulioanza nchi nzima jana Julai 30, 2012.
Kiongozi wa wanafunzi walioandamana jana jijini Dar es Salaam, Christofa Msifuni Msuya wa darasa la saba, shule ya msingi Bwawani, akizungumza kwa niaba ya wenzake kwenye ofisi za Afisa Elimu wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 30, 2012.
Add caption
Wanafunzi wa shule za msingi Bwawani na Kijichi, zajijini Dar es Salaam, wakiamnadmana jana kupinga kile walichokiita kuvurfughwa kwa haki ya mtoto ya kupata elimu, na hii ni kufuatia mgomno wa walimu ulioanza jana nchi nzima. Wanafunzi hao waliandamana hadi urefu wa kilomita 10 kutoka shuleni kwao hadi ofisi ya Afisa Elimu wa Manispaa ya Temeke, ziliko shule hizo, jirani na uwanja wa taifa ili kufikisha kilio chao.

Wanafunzi wakiwa wanaelekea ofisi ya Mkuu wa wilaya
Wanafunzi wa shule za msingi Vwawa wakiwa wanapiga vidumu huku wakielekea ofisi ya mkuu wa wilaya ni Baada ya walimu kugoma.
Moja ya wanafunzi wa shule ya msingi Meta baada ya kuona walimu hawajaingia darasani yeye alichukua jukumu la kuwafudnisha wenzake
Wanafanzi wa darasa la saba shule ya msingi Meta wakiendelea kupeana mazoezi ya masomo mbalimbali baada ya waalimu wao kugoma kuingia madarasani
Wanafuzi wapo makini kumsikiliza mwanafunzi mwenzao
Mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi muungano akiwa nje ya shule akichezea mchanga maana walimu wamegoma
Picha na Arithy via Mbeya Yetu blog
Mwalimu wa Shule ya Msingi Mmoja, Salma Mtili akisahihisha daftari la mwanafunzi wa darasa la nne wa shule hiyo licha ya rais awa Chama cha Walimu Tanzaniza (CWT) kutangaza mgomo wa walimu nchi nzima.
Picha na Habari Mseto Blog 


Wanafunzi wa shule ya msingi Ipembe, Nyerere, Unyankindi na Singidani katika Manispaa Singida (picha na Nathaniel Limu)