PORTO KUMUUZA MOUTINHO KWA PAUNDI MILIONI 31.

Moutinho.
KLABU ya Porto imethibitisha kuwa inaweza kumuuza mchezaji wake Joao Moutinho lakini wameionya klabu ya Tottenham Hotspurs ambayo inamuwinda mchezaji huyo kuwa watatakiwa kulipa kiasi cha paundi milioni 31.5 kama wanamuhitaji kiungo huyo. Moutinho amekuwa mchezji tegemeo kwa klabu na nchi yake ambapo meneja mpya wa Spurs Andres Villas-Boas ambaye ameshawahi kumfundisha kiungo huyo mwenye miaka 25 ni chaguo lake kubwa analohitaji. Kwasasa kocha huyo bado hajafanya mawasiliano na Porto kuhusiana na mchezaji huyo lakini wameonyesha nia ya kumhitaji mchezaji huyo na wako tayari kuanza mazunguzo kuhusu kiwango hicho cha fedha kilichowekwa na porto. Meneja wa Porto Votor Pereira amesema kuwa bado hajazungumza na Villas-Boas kuhusiana na suala hilo lakini anaonekana kumtaka mchezaji huyo na wao wanamhitaji lakini katika soka kama ikifikia wakati kama huu timu inakuwa haina jinsi bali kumuuza na kuiletea faida klabu. Spurs inamuhitaji Moutinho ili kuziba pengo la Luka Modric ambaye anaweza kuondoka msimu huu baada ya vilabu vya Real Madrid na Paris Saint Germain zikiitafuta saini yake kwa udi na uvumba.