Emmanuel Almunia. |
KLABU ya Arsenal imesema
kuwakipa wake wa zamani Manuel Almunia amejiunga na klabu ya Watford
inayoshiriki ligi daraja pili nchini Uingereza. Almunia ambaye amepewa
mkataba wa mwaka mmoja anakuwa mmoja kati ya wachezaji wapya saba
waliosajiliwa na Watford ambayo inanolewa na kocha Gianfranco Zola.
Taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu ya Arsenal ilithibitisha kuwa
ni kweli klabu hiyo imemwachia Almunia kwenda Watford kwa mkataba wa
mwaka mmoja. Almunia amecheza michezo 175 akiwa na klabu ya Arsenal
ukiwemo mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2006 dhidi ya
Barcelona ambao aliingia kama mchezaji wa akiba lakini alipoteza namba
katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo kwa Wojciech Szczesny ambaye ni
raia wa Poland. Watford ambayo katika siku za karibuni ilinunuliwa na
familia ya Pozzo ambao pia wanamiliki klabu ya Udinese inayoshiriki Ligi
Kuu nchini Italia na Granada ya Hispania, pia imewasajili Fitz Hall,
Almen Abdi, Matej Vydra na Steve Leo Beleck.