Hata hivyo alisema kuwa video ya ngoma hiyo inaanza kupigwa picha kesho na wanahitaji audio na video ziweze kutoka kwa pamoja.
“Uwezi amini nimefanya ngoma ya Kurap na najua watu watu watanichukulia tofauti sana lakini najua uwezo wangu ni mkubwa katika kila aina ya muziki ninaotaka kufanya, na hii kazi itakuwa na uwezo wa kusikilizwa popote pale kutokana na uzuri wake, ” alisema.
Hata hivyo aliongeza kuwa baada ya ngoma hiyo atakuwa katika maandalizi yake mengine ya kutoa kazi mpya, ambayo bado hajajua ipi itakayokwenda hewani kwani amefanya kazi mbili na wasanii mahiri wa taarubu moja na Hadija Kopa na nyingine na Mzee Yusuph.
“Kuna ngoma mbili ambazo sijajua ipi itaanza kwenda hewani hivyo nahitaji kukaa na wadau ili waweze kunishauri niitangulize ipi ingawa ngoma zote ni kali sana,” alisema.