DOS SANTOS KUWAKOSA BRAZIL KATIKA FAINALI YA OLIMPIKI WEMBLEY.

Giovani Dos Santos.
MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya taifa ya Mexico Giovani dos Santos atakosa mchezo wa fainali ya soka ya olimpiki baina ya timu yake na Brazil mchezo ambao utafanyika katika Uwanja wa Wembley jijini London, Uingereza. Kocha wa Mexico Luis Fernando Tena alithibitisha kumkosa mchezaji wake huyo katika mchezo huo wa fainali lakini akadai kuwa hayakuwa majeraha makubwa sana ingawa hatakuwemo katika kikosi chake kitakachokuwa kikiwania medali ya dhahabu. Tena aliendelea kusema kuwa ilikuwa ni ndoto ya mchezaji huyo kucheza mchezo huo wa fainali jijini London kwasababu ndio mahali anapoishi na anacheza katika timu ambayo inatoka katika mji huo lakini hilo halitawezekana kwakuwa itamchukua kama wiki mbili ili aweze kupona majeraha yanayomsumbua. Mexico watakuwa na kazi ya ziada katika mchezo wao huo haswa ikizingatiwa kuwa wapinzani wao Brazil watakuwa na nyota wao wote kama Neymar, Oscar na Leandro Damiao ambaye anaongoza kwa ufungaji katika michuano hiyo akiwa na mabao sita mpaka sasa. Brazil kama ilivyo kwa Mexico wote watakuwa wakifukuzia medali za kwanza za dhahabu katika michuano hiyo