GADNER G. AJA NA MASKANI TIMES FM.....KITAA WANASEMA ATALIPWA MILIONI 5 KWA KILA MWEZI

Aliyekuwa mtangazaji wa Clouds FM katika kipindi cha Jahazi, Garder G Habash aka Captein anatarajia kuanza kutangaza tena Jumatatu ijayo kupitia kituo cha radio cha Times FM 100.5 cha Dar es Salaam.
Kipindi chake kiitwacho Maskani kitakuwa kikiruka kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa  kuanzia saa 10 jioni hadi saa 1 usiku.

Gadner akiongea machache baada ya kutambulishwa Times FM
Kuna tetesi za mtaani ambazo hazijathibitishwa rasmi zinazosema kuwa mtangazaji huyo atakuwa akilipwa shilingi milioni 5 kwa mwezi.

Kama tetesi hizo zitakuwa na ukweli, Gadner atakuwa mtangazaji wa radio anayelipwa pesa nyingi zaidi nchini.



Kipindi chake kinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na kipindi chake cha zamani,  Jahazi cha Clouds FM ambacho kwa sasa huendeshwa na Arnord Kayanda, Wasiwasi Mwabulambo na Ephraim Kibonde.

Hata hivyo Clouds FM watakuwa na advantage katika mikoa mingine ambayo Times FM haisikiki.

Picha ya pamoja ya baadhi ya watangazaji wa Times FM. Kutoka kushoto ni: Gadner, Schola, Natasha, Ndimbo, Dida na Joet.
 
Kwa upande wa Dar es Salaam, Maskani ina nafasi kubwa ya kuchukua wasikilizaji wengi wa Jahazi hasa wanaosikiliza radio wakiwa majumbani.

Times FM wana disadvantage ya frequency walinayo ya 100.5 ambayo gari nyingi haizifikii na hii ni kwasababu kuna wasikilizaji wengi jijini Dar es Salaam wanaosikiliza radio kwenye magari.