Lulu Asema "Jamani Nimemiss Uraiani"
|
LULU |
MCHEZA sinema wa Bongo aliye nyuma ya nondo katika Gereza la Segerea,
jijini Dar es Salaama kwa madai ya kuhusika na kifo cha Msanii Steven
Kanumba, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kuwa amepamisi sana uraiani.Akizungumza na mwandishi wetu Agosti 13, mwaka huu katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu ambako kesi yake inaendelea kutajwa, Lulu alisema
amemisi vitu vingi vya uraiani, ikiwemo mitaa ya Sinza na Kinondoni
alikozoea kwenda kujiachia, pia anawakumbuka sana mashosti wake akina
Diana Kimaro ‘Pacha wa Lulu’.
“Nimekumisi sasa… (anataja jina la mwandishi), pia nimewamisi watu wote
huko uraiani, nimewamisi mashosti wangu jamani, nimemisi sehemu
nilizokuwa napenda kutembelea,“ alisema Lulu.
Lulu akionesha uso wa uchangamfu alisema anafurahi sana anapoona watu
wanaofika mahakamani hapo ni baadhi ya marafiki zake na ndugu.
“Ukikaa kule (gerezani) unawakumbuka watu wengi, sasa ukija hapa
(mahakamani) unapowaona watu mbalimbali unaowafahamu kidogo unafarijika,
unakuwa mwenye amani siku hiyo,” alisema Lulu.