
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Loveness Witson Mwaseba amefunguka kuwa hataki kutoa penzi kwa maprodyuza na madairekta wakubwa ili apate umaarufu kwa kupewa upendeleo na kuchezeshwa filamu nyingi kama wafanyavyo mastaa wengine. Loveness alifunguka kuwa kila kukicha huwa anapata usumbufu wa baadhi ya maprodyuza na madairekta wakimtaka kimapenzi ili wampe nafasi ya kucheza movie zao na baada ya hapo wamfanyie promosheni kwenye vyombo vya habari.
“Siko tayari kusaka umarufu kwa kugawa penzi kutoka kwa maprodyuza au madairekta ambao wamekuwa wakinitaka kila siku nifanye hivyo,” alisema Lovenes.