JAMBO MOJA USILOLIJUA KUHUSU MUHOGO MCHUNGU.....


Ukiniamsha usingizini ukaniambia nikutajie majina 5 ya wasanii wa sanaa ya maigizo nchini Tanzania,nina uhakika kabisa kwamba miongoni mwa majina hayo bila shaka nitakutajia Muhogo Mchungu. 

Ni muigizaji mkongwe katika sanaa na ambaye naamini endapo waigizaji wanaochipukia wangechukua muda wao kutaka kujifunza kutoka kwake,basi wangefaidika na mengi sana.

 Ninachokipenda zaidi ni jinsi anavyoweza kuuvaa uhusika katika namna ambayo ni halisi(natural acting).Ukimtazama unaona uhalisia wa maisha na kile anachokiigiza.Naam,huo ndio uigizaji.
 
Lakini ungeniuliza jina lake,ningebaki kama Bubu.Macho yangenitoka na akili kunizunguka.Nisingelijua.Ninalolijua mimi ni jina lake la kisanii…Muhogo Mchungu.

 Lakini alipofika pale Amaya Beauty Salon & Spa na kuketi na Salama Jabir na wenzake John na Muba,aliulizwa jina lake.Amelitaja zaidi ya mara moja.Ajabu,ninapoandika hapa bado nakumbuka majina mawili tu ya mwanzoni yaani Abdallah Said…mengine je?

Yawezekana nawe ukawa kama mimi kwamba hukuwahi kulijua jina lake halisi.

Msikilize hapa Mhogo Mchungu akiongelea mengi.Alah..kumbe yeye na wale watoto wa Jangwani ni..

Thankx, Celebraty bongo

MSIKILIZE MUHOGO MCHUNGU