Picha ya Lord Eyez baada ya kukamatwa eneo la tukio
Habari tulizonazo zinadai kuwa bado polisi wanamshikilia rapper huyo maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kwamba tukio hilo lilitokea jana maeneo ya Kinondoni Manyanya.
Pia kuna taarifa kuwa Lord Eyez alikuwa pamoja na kijana ambaye husema ni mtoto wa aliyewahi kuwa rais wa Zanzibar Salmin Amour (ukweli ni kuwa si mwanae bali aliwahi kuishi na familia hiyo) ambao wote wanashikiliwa. Kijana huyo amewahi kuhusika katika matukio mengine kama hayo ya wizi wa vifaa vya magari.
Jana kupitia Twitter, Ommy Dimpoz aliandika, “Mwizi wetu kasema vitu viko chimbo tandale…naona km naota#LordEyesMwiziWaPowerWindow.”
“Kinachoniuma alidhamiria coz gari yangu anaijua na mizinga akinipiga huwa namtoa.”
“Sio mm tu wiki iliyopita alimuibia kerry mfanyakazi wa clouds tv
huku akishirikiana na mtoto wa kigogo mkubwa ambae wanavuta nae madawa.”
Tukio hilo limevuta hisia za wengi hususan wasanii wenzie ambao wengi wanashindwa kuamini iwapo rapper huyo amefikia hatua ya kuhusika na matukio ya wizi.
“Hajapatwa na hatia bado lakini mambo ya huu mji yanafahamika na kupata taarifa sahihi ambazo mamlaka huwa zinakwepa kuzifanyia,” aliandika MwanaFA.
Tukio tayari liko mikononi mwa polisi na uchunguzi unaendelea.
USHAIDI WA TUKIO:
.
.
.
.