Mwananchi wa sumbawanga akitoa maoni juu ya katiba mpya katika viwanja vya maktaba ya mkoa wa Rukwa leo |
Wananchi wa sumbawanga leo wamepata
nafasi ya kutoa maoni kuhusu mchakato wa kupata katiba mpya,mbele ya
wajumbe wa tume ya katiba, wananchi wamepata fursa ya kuchangia yale
wanayodhani yanafaa kuwemo katika katibu mpya.
Wapo waliochangia kwa kuongea pia wapo waliochangia kwa njia ya maandishi
Jambo Kubwa ambalo limejitokeza katika
mchakati huo ni suala la dini wengi watoa maoni wamekuwa wakizungumzia
suala la dini , mfano mtu mmoja alisema angependa kwenye katiba
ingeonyesha kuwa siku ya kuabudu waislamu ijumaa kuwa ni siku ya
mapumziko kama ilivyo siku ya jumapili kwa wakristo.
Mama mmoja aliyejitambulisha kuwa ni
mwalimu yeye alisema kama waislamu wanataka kuwepo na mahakama yao hivyo
haina budi na wakristo nao wapewe mahakama yao mama huyo aliweza
kumnukuu baba wa taifa akisema "Mwalimu Nyerere alisema serikani haina dini" hivyo akahoji kama waislamu wakitaka mahakama yao serikari itakuwa na dini moja hayo ni baadhi ya maoni ya mama huyo