PENZI LA NEY WA MITEGO LAMCHANGANYA BINTI WA 20 PERCENT
MWIGIZAJI
wa kike katika ya tasnia Bongo Movies Asfa Omary Neema 20% ameshindwa
kuficha hisia zake pale alipodai kuwa pamoja na umri wake mdogo
anamzimia sana msanii wa Bongo fleva, Ney wa Mitego. "Siyo
siri ,nampenda sana Ney wa Mitego na natamani awe mume wangu wa ndoa
hata kesho kama akikubali, kama ingekuwa wasichana tunaruhusiwa
kuwatongoza wanaume na kuolewa nao basi mimi ningekuwa wa kwanza kwa
Ney, ana mvuto na shababi" Neema 20%.
Neema
ni msanii aliyevuma na kuibuka kupitia filamu ya 'Furaha Iko Wapi'
iliyotungwa na msanii wa muziki wa Bongo fleva Hamis Kinzasa "20
Percent" amedai kuwa anampenda mwanamume anayejiamini na kuwa mtanashati...
Anadai kuwa hizo sifa anaziona kwa msanii Ney pekee na si mtu mwingine, na atafanya kila
juhudi ili aweze kuishi na msanii huyo