SERIKALI imepiga marufuku mihadhara ya kidini nchi nzima kwa siku 30
ikiwa ni moja ya hatua ya kukabiliana na machafuko ya kidini
yanayolinyemelea taifa.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel
Nchimbi alitangaza hatua hiyo ya Serikali jijini Dar es Salaam jana,
wakati akizungumza na waandishi wa habari.Waziri Nchimbi
alisisitiza kuwa Serikali pia inafanya uchunguzi ili kubaini kama
vurugu hizo zina mkono wa makundi ya nje ya nchi.
Alisema kuwa, Serikali sasa haitawabembeleza watu wanaoeneza chuki za kidini kwa sababu ni wajibu wake kulinda amani kwa wananchi wake.
Waziri huyo alieleza kusikitishwa na vurugu zilizotokea juzi Ijumaa maeneo mbalimbali jijini baada ya baadhi ya Waislamu kujiandaa kuandamana kwenda Ikulu kushinikiza kutolewa rumande kwa kiongozi wao, Sheikh Issa Ponda.
Waandamanaji hao pia walipinga tukio la kukojolewa kwa kitabu kitakatifu cha Kurani na mtoto lililotokea mwanzoni mwa wiki eneo la Mbagala.
“Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ametangaza juzi kusitisha mihadhara ya nje kwa siku 30. Na mimi natumia fursa hii kutangaza kusitisha mihadhara hiyo kwa nchi nzima kwa siku 30, hadi tutakapoona hali imetulia,” alisema Nchimbi.
Waziri Nchimbi alikiri pia kwamba, Serikali imekuwa ikikosea kuwakamata watu wanaofanya vurugu wakati wa maandamano na kuwaacha wanaoshawishi na kuwezesha maandamano hayo.
Tumegundua kwamba, tulikuwa hatufuati sheria kwa kuwakamata tu
wanaotenda. Ndiyo maana baada ya upelelezi tukaona kuwa wasaidizi wake
(Ponda), waliwashawishi watu waandamane kwenda Ikulu ,au gerezani ili
wamtoe (Ponda) rumande,” alisema Dk Nchimbi.
Alisema kuwa, Serikali sasa haitawabembeleza watu wanaoeneza chuki za kidini kwa sababu ni wajibu wake kulinda amani kwa wananchi wake.
Waziri huyo alieleza kusikitishwa na vurugu zilizotokea juzi Ijumaa maeneo mbalimbali jijini baada ya baadhi ya Waislamu kujiandaa kuandamana kwenda Ikulu kushinikiza kutolewa rumande kwa kiongozi wao, Sheikh Issa Ponda.
Waandamanaji hao pia walipinga tukio la kukojolewa kwa kitabu kitakatifu cha Kurani na mtoto lililotokea mwanzoni mwa wiki eneo la Mbagala.
“Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ametangaza juzi kusitisha mihadhara ya nje kwa siku 30. Na mimi natumia fursa hii kutangaza kusitisha mihadhara hiyo kwa nchi nzima kwa siku 30, hadi tutakapoona hali imetulia,” alisema Nchimbi.
Waziri Nchimbi alikiri pia kwamba, Serikali imekuwa ikikosea kuwakamata watu wanaofanya vurugu wakati wa maandamano na kuwaacha wanaoshawishi na kuwezesha maandamano hayo.
“Huo ndiyo uamuzi mpya wa Serikali.
Anayeshawishi, anayefanikisha na anayewezesha, wote watakamatwa.