Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
7/10/2012
TUME ya Mabadiliko ya Katiba (kesho jumatatu,terehe8.Oktoba,2012) inatarajia kuanza awamu ya tatu
ya kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu KatibaMpya katika Mikoa tisa (9) ikiwemo saba (7)
ya Tanzania Bara na miwili ya Zanzibar.
Taarifa iliyotolewa (leo jumapili tarehe 7. Oktoba, 2012) Jijini Dar es Salaam, na Katibu wa Tume
hiyo, Assaa Rashid na kusambazwa katika vyombo vya habari inaitaja Mikoa hiyo kuwa ni Mtwara,
Kilimanjaro, Iringa, Singida, Njombe, Rukwa, Tabora, ambayo yote ni ya Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo inasema pia Tume hiyo inatarajia kuitisha mikutano yake katika mikoa miwili
ya Zanzibar, ambayo ni Kaskazini Unguja na Kaskazini Pemba.
Aidha taarifa hiyo inaongeza kuwa katika Mkoa wa Mtwara, Tumei taanza na Wilaya ya Nanyumbu,
katika Mkoa wa Kilimanjaro Tume itaanza na Wilaya ya Moshi Mjini, katika Mkoa wa Iringa Tume
itaanza katika Wilaya ya Mufindi. Kwa Mkoa wa Singida, Tume itaanza na Wilaya ya Iramba, wakati
Mkoani Njombe , Tume itaanza na Wilaya ya Ludewa.
Taarifa hiyo pia inaeleza kuwa katika Mkoa wa Rukwa Tume itaanzia katika Wilaya ya Nkasi, Mkoa wa
Tabora Tume itaanza katika Wilaya ya Kaliua, Mkoa wa Kaskazini Unguja Tumeitaanza katika Wilaya ya
Kaskazini “A” na Mkoa wa Kaskazini Pemba Tume itaanza katika Wilaya ya Wete.
Tume hiyo pia inawaomba wananchi kuhudhuria mikutano itakayoitishwa na Tume na kushiriki
kikamilifu katika kutoa maoni yao binafsi kuhusu Katiba Mpya.
Taarifa hiyo pia inawasisitiza wananchi wamikoa hiyo hasa wanawake na watu wenye ulemavu kutumia
fursa ya kushiriki katika mikutano hiyo inayoitishwa na Tume ili kutoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya.