YALIYOJIRI TOKA MAHAKAMA YA ARUSHA KATIKA RUFAA YA GODBLESS LEMA



Aliyekua mbunge wa Arusha Mjini(CHADEMA)Godbless Lema
------------------------------------------------------------------
 
YALIYOJIRI  TOKA ARUSHA
Muda huu ukumbi wa mahakama umefunguliwa, watu wamejaa ndani ya ukumbi.
Lissu ameshawasili, anasalimiana kwa kukumbatiana na Alute.MORE UPDATES:
  - Bado ukumbi umetulia, namwona Cecilia Pareso ameingia. - Kamanda Lema ameingia, namwona na wapinzani wake kwenye kesi hii Musa Mkanga na Agness Mollel nao ndani ya nyumba. - Majaji wameingia. Kesi imeanza... - Method Kimomogoro na Lissu wanawakilisha rufaa. - Upande wa pili unawakilishwa na Modest Akida na Alute. - Wote wapo tayari kuendelea na shauri. Chande: Leo waanasikiliza pingamizi za awali kwanza

Chande: Kabla hatujaanza kusikiliza, mawakili wote wawe na right of audience.

  Kimomogoro: Upande wa rufani tuna uhalali wa kusimama mbele ya rufaa kwa zaidi ya miaka kumu

  Alute: Nina uhalali tangu 1985 Lissu: Nimekuwa wakili tangu 2003, hivyo nina zaidi ya miaka mitano.
 ------------------------------------------------------------------------
Chande:
Leo waanasikiliza pingamizi za awali kwanza

Kabla hatujaanza kusikiliza, mawakili wote wawe na right of audience.

Kimomogoro: Upande wa rufani tuna uhalali wa kusimama mbele ya rufaa kwa zaidi ya miaka kumi

Alute:
Nina uhalali tangu 1985

Lissu: Nimekuwa wakili tangu 2003, hivyo nina zaidi ya miaka mitano.

 ----------------------------------------------------------------------
Majaji naona wanashauriana baada ya kusikiliza maelezo ya TL kuwa ana haki ya kusikilizwa kwenye mahakama hii tukufu

Alute: Rufaa ni batili on a decree of the high court. Decree haikubaliani na hukumu.

Reference to page no 957/958 kifungu cha 14 sheria ya uchaguzi. Mkurugenzi wa uchaguzi azingatie sheria ya uchaguzi.

Decree haijaandikwa kama inavyotakiwa na sheria.

Na katika hili tumeambatanisha hukumu ya mahakama hii tukufu iliyotolewa mwezi wa tano dhidi ya Gesud Bajuta.
-----------------------------------------------------------------------

Kesi hii imeelekeza kuwa hii decree inatakiwa iwe na format ipi. Kwenye ukurasa wa sita hadi nane.

Kwenye hii kesi tar ya decree ilikuwa imekosewa. Haya ni maelezo ya Alute yanaendelea.

Mahakama ilikumbushia umuhimu wa kuzingatia decree.

Kesi iliyopo mbele yetu decree imekosewa, haina baadhi ya maneno kama given under my hand in a seen of the court.

Decree haionyeshi ni lini imechukuliwa. Imekiuka kanuni ya tisa ya kanuni ya masijala ya mahakama.

Kanuni ya tisa "All summons shall be seen of the court. And should show when the order was distracted"

-------------------------------------------------------------------------
Alute: Hii decree ina hitilafu, amekiri kuwa ina saini ya jaji, lakini haina muhuri wa mahakama. Bila muhuri mheshimiwa, hii decree is like a piece of paper. Decree lazima iwe kwenye formalities, na moja ya hiyo formalities ni lazima decree iwe na muhuri to show the seen of the high court. Sign peke yake haina maana.

Hii decree ni batili si makosa ya waleta rufaa bali makosa ya mahakama. Lakini pia waleta rufaa walitakiwa kuchunguza vizuri makaratasi kama yamekidhi rufaa.

Kwakuwa hii decree ni batili, basi na rufaa nayo itakuwa batili.

Chande: Alute elewa kwamba mwisho wa siku ni mambo ya mamlaka. Na aliyetoa hukumu ni jaji Rwakibarila, rufani ilisainiwa na yeye. Bado unabisha kwamba siyo mamlaka ya ofisi ya mahakama?

Alute: Bila muhuri wa mahakama the answer is no!

Chande: Kuhusu kasoro ya muda, order twenty sect. 7 haionyeshi suala la muda.

Alute
: Lina uzito mheshimiwa, kwa sababu hakuna certificate of delay.

Chande anamwuliza Alute kwa maoni yake kama ameona ni batili, atoe ushauri wa adhabu mbadala.

Alute anasema kuna makosa huwa hayana adhabu mbadala.

Kweli hii kesi ya uchaguzi uchaguzi, lakini mahakama hii kwa kukosa decree of the court ilifuta kesi ya Fortunatus Machana, panga hilo hilo litumike kwenye rufaa hii.

 -----------------------------------------------------------------

 Kimomogoro: Ningeanzia alipoishia Alute.

Anasema mwenyewe aliandika barua kuomba decree haikujibiwa. Kama yake haikujibiwa ya kwetu ingejibiwa vipi?

Mtaona kwamba drawn order imekuwa sealed. You need circumstance kusikiliza shauri hili.

Barua alizoomba corrective decree iliomba point no 4, haikuzungumzia lingine.

Msomi mwenzetu alisema marekebisho haya ili ayatumie kwenye shauri hili.

Kwa bahati mbaya barua zote hazikunukuliwa kwetu.

Msomi mwenzangu amesema hakukuwa na wajibu wa kuensure the record proper. Wakati kanuni zinamwelekeza hivyo.

Waheshimiwa tunaomba muelekeze kama mlivyomwelekeza msomi mwenzangu.

Alute hajazungumzia authorities tulizoambatanisha zinazoelezea kusahihisha decree. Tunaamini amechenga kwa makusudi

Kimomogoro:


Jukumu ni la jaji aliyetoa uamuzi kuhakikisha kuwa decree imetengenezwa. Tumetoa pia kesi ya mausi vs Arusha general store. Mahakama ilitoa mwongozo kuhusu aina ya kanuni, moja ni mandatory na directory.

Mahakama ilisisitiza kwamba kanuni za mwongozo hazitaathiri muendelezo wa kesi. Kasoro zilizotajwa kwenye hiyo zote ni clerical error.

Makosa mengine ni ya muundo'given under my hand in a seal of the court' na date of extraction, imefutwa na GN no 6 ya mwaka jana

Mheshimiwa jaji aliridhika ni hii decree,akaweka mkono wake, kwahiyo imekamilika. Kama jaji aliridhika kimakosa, sisi hatuna makosa.

Kuhusu reg.Rule inahusika na masijala. Decree ikishapata sign ya jaji kinachofuata ni kusikilizwa.

Kama decree ni batili basi Mteja wetu bado ni mbunge wa Arusha, kwasababu hakuna kilichomtengua.

MWENDELEZO  UNAKUJA.......
ASANTE  JAMII FORUM