"LAZIMA NIYAANGALIE MAKALO YANGU KAMA BADO YAPO KILA NIAMKAPO.NIKIYAKOSA LAZIMA NIOMBEWE"...AUNT LULU


ALIYEKUWA mtangazaji wa Runinga ya C2C ambaye kwa sasa ni mwigizaji, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’, ametoa kali ya mwaka baada ya kufunguka kuwa siku akiamka asubuhi na kukuta makalio yake hayapo, atakimbilia  kwa mchungaji kuombewa.


Akizungumza kwa  mbwembwe, mtangazaji huyo ambaye ana vituko lukuki, alisema kila siku anapoamka asubuhi, lazima aangalie kama makalio yapo ndiyo mambo mengine yafuatie. 



“Jamani nikiamka kitandani, kabla ya kuoga na kupiga mswaki cha kwanza najitazama nyuma kama hili nililojaliwa na Mungu lipo na nisipolikuta, nakimbilia kwa mchungaji kuombewa fasta,” alisema Lulu.

Lulu aliongeza kuwa, hakuna kitu anachokipenda katika mwili kama makalio yake, hivyo hayupo tayari kuishi bila ya hayo makalio kwani ndiyo kila kitu katika mwili wake.


“Haya ndiyo kila kitu, usiniulize kwa nini nayapenda sababu naijua mimi mwenyewe,” alisema.