DIAMOND AFANANISHWA NA MWANAUME MSHAMBA, LIMBUKENI NA ALIYEKURUPUKIA MAPENZI UKUBWANI


 

KAMA USHAMBA NI SOMO BASI MFANO NI HUU HAPA!!!.
USHAMBA. Binafsi namshabikia sana huyu Msanii but I cant take it anymore!, Awali ya yote tuelewe kwamba kumdhalilisha mwanamke yeyote na kwa namna yoyote ni sawa na kumdhalilisha mama yako mzazi!,

Mambo ya kuanza kurekodiana kwenye maongezi yaliyo private na kuyasambaza binafsi naona ni kuvuka mipaka na Ushamba uliopitiliza,

DIAMOND unaimba nyimbo nzuri za mapenzi lakini sasa una-prove Ushamba juu ya Mapenzi yenyewe,kifupi hakuna mtu anayekulazimisha uwe na mrembo gani kimapenzi kwani wewe ni mtu mzima maliza wanawake wote duniani ikiwezekana tembea mpaka na Mamba wa kwenye Mabwawa,hiyo ni hiari yako, ila unapopeleka hewani sauti ya maongezi private na wema aidha kwa kutafuta kuongeza umaarufu,this is rubbish!!!,

Kwa haraka haraka ukimsoma diamond unagundua kuwa ni wale wanaume ambao hawakuwahi kubahatika kupendwa na wanawake wazuri,sasa wanapokuja kushika pesa au umaarufu ndio inakuwa siraha yao ku prove kwenye jamii kwamba hata nao wanaweza.

Yaani Diamond kushobokewa na madem wazuri kwake ni kama ngekewa ndiomaana anaingia kichwa kichwa.

PENNY usisahau kwamba huyu wema alikuwa rafiki yako na ukamchukulia Bwana,tena bwana mwenyewe ni huyu mtoto wa kiswazi ambaye Mapenzi yanampeleka puta!,anayedhihirisha ulimbukeni wake kwenye jamii.
 
Leo kwa ushirikiano wako na Diamond umemuanika msichana mwenzako kumdhalilisha,ok tia maji kichwa chako hii ni Bongo soon utanyolewa na tutaandika hapa hapa.

WEMA, Sasa ukae chini ujifunze kwamba mitoto ya Kiswazi mingi milimbukeni,wewe ni binadamu na hujakamilika basi jaribu kujikamilisha kwa kupunguza makosa,sina maana ya kwamba nakutetea wewe bali binafsi sipendezwi na KUDHALILISHWA KWA MWANAMKE YEYOTE!

KIOO CHA JAMII :
Hapa hakuna kioo,ni heri kuzamisha sura kwenye tundu la choo ukiamini kwamba utaiona taswira yako kuliko kuwapa dhamana wasanii malimbukeni. 
Credit: Sheria ni Msumeno