Mrembo
huyu aliyejitambulisha kwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu kimojawapo
mjini Iringa akilia baada ya kupokea kichapo kutoka kwa mwanamke
mfanyabiashara eneo la Miyomboni mjini Iringa baada ya kuiba viatu
vya mtumba na kuficha kwapani
Hapa akimpigia simu mpenzi wake ili aweze kumkomboa baada ya kutakiwa kulipa Tsh 50,000 kwa viatu pea mbili alizoiba .
----------------------------------------------------
Tukio
la mrembo huyo kupokea kichapo na kuvuliwa nguo na kupokonywa
simu yake na mikoba zaidi ya mitano pamoja na kiasi cha TSh 15,000
ambazo alikuwa amezihifadhi limetokea jumapili wiki hii katika eneo
la Miyomboni mjini Iringa.
Akielezea
juu ya mkasa huo wa aina yake leo mfanyabiashara huyo mama
Masawe alisema kuwa eneo hilo amekuwa na kawaida ya kuibiwa viatu
katika duka lake la viatu vya mtumba .....
Mama huyu anadai kuwa mbali ya kukamatwa
kwa mrembo huyo bado amepata kukamata vijana zaidi ya wawili
watanashati ambao wamekuwa wakifika na kujifanya wakichagua viatu na
kuishia kuiba na kutoweka .
Binti huyo ambaye ni mwanachuo alifika dukani hapo
na kuanza kuchagua viatu akijifanya ni mteja .....
Baada
ya kuona muuza duka ameangalia pembeni, binti huyo alichukua
pea mbili za viatu na kuzificha kwapani asijue kwamba pembeni
kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa akimwangalia....
Alipoaga
na kutaka kuondoka
ndipo timbwili la kichapo lilipoanza kwa mrembo huyo ambae aliomba
asipelekwe polisi na asipewe adhabu kubwa kwa kuwa
ana ujauzito wa miezi mitatu tumboni.
Alisema
kuwa kutokana na maombi ya mrembo huyo kupunguziwa adhabu hakuweza
kumfikisha polisi zaidi ya kumpa kichapo cha kufa mtu na kumpokonya
mali zote alizokuwa ametoka kuiba katika maduka ya Miyomboni mjini
hapa pamoja na simu yake ya kiganjani .