Watumiaji, watoa huduma, wakala wa makampuni ya simu za mkononi na wananchi kwa ujumla wamekumbushwa kuwa ni kosa kisheria kutumia au kuwezesha kutumiwa kwa namba ya simu ambayo haijasajiliwa. Akitoa tamko la pamoja kwa umma la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na Makampuni yanayotoa Huduma za Simu kuhusu Usajili wa namba za Simu za Mkononi Tanzania Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma amesema ni kosa la jinai kutumia namba ya simu isiyosajiliwa na adhabu yake ni faini ya shilingi laki 5 au kifungo cha miezi mitatu.
Ameongeza
kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 130 cha Sheria ya Mawasiliano ya
Elektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010, mtu yeyote ambaye anauza au
anatoa kwa namna yeyote ile namba namba ya simu bila kuisajili
anatenda kosa la jinai na adhabu yake ni faini ya shilingi 3,000,000 ai
kifungo cha miezi 12 au vyote.
Aidha
Prof. Nkoma amewashauri watumiaji wa simu za mkononi na wananchi
kuunga mkono juhudi zinazofanywa ili kufanikisha usajili wa namba za
simu kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza amani na usalama na
kuharakisha maendeleo ya sekta nay a Taifa kwa ujumla.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Prof. John Nkoma akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutoa tamko la pamoja
kwa umma la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na Makampuni yanayotoa
Huduma za Simu kuhusu Usajili wa namba za Simu za Mkononi Tanzania
ambapo amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ikishirikiana na
makampuni ya Simu na vyombo vya usalama imeanza kampeni endelevu yenye
lengo la kuwabaini wote wanaohusika na uvunjifu wa sheria ili kuwalinda
watumiaji wema na jamii kwa ujumla kwa ajili ya kuimarisha usalama na
kuleta maendeleo na ustawi wa wananchi.
Mkurugenzi
Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania Diego Gutierrez
akielezea jinsi kampuni yake ilivyojidhatiti katika kutoa huduma kwa
wateja na kuhakikisha kila namba ya simu inayotolewa na kampuni ya simu
ya Tigo inasajiliwa kwa mujibu wa kifungu cha 102 (1) cha Sheria ya
mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA).
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma (wa
tatu kushoto) akiwa meza kuu na Wakurugenzi Watendaji Wakuu wa Kampuni
yanayotoa huduma za simu nchini.
Baadhi maafisa mbalimbali na wawakilishi wa makampuni yanayotoa huduma za simu nchini katika mkutano huo.
Sehemu ya wawakilishi mbalimbali wa vyombo vya habari nchini.