MHINDI mwenye uraia wa India, Srinivasa Rao Talluri, 36 anayedaiwa
kumuua Mwalimu Elizabeth Mmbaga wa Shule ya Msingi Atlas, jijini Dar es
Salaam amejiua Aprili 17 mwaka huu katika Hoteli ya Transit iliyopo
Karakata.
Talluri ambaye alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya vinywaji
vikali ijulikanayo kwa jina la Moan’s Drinks Ltd iliyopo Oysterbay, Dar
maiti yake ilikutwa chumbani saa mbili asubuhi na inadaiwa alijiua kwa
kunywa sumu ambayo mabaki yake yamepelekwa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa
Serikali kwa uchunguzi.
Habari za kipolisi zimesema kuwa baada ya wafanyakazi wa Hoteli ya Transit jijini Dar kugundua kuwa Mhindi huyo amekufa, walitoa taarifa polisi ambao walifika na walipochunguza chumbani, walikuta kuna pombe aina ya Pushkin chupa tatu, chupa yenye sumu ya kuulia wadudu, chips na maziwa glasi moja.

Marehemu Elizabeth Mmbaga enzi za uhai wake.
Inadaiwa kwamba Mhindi huyo aliachishwa kazi katika kampuni hiyo
Aprili 2, mwaka huu baada ya kugundulika kuwa alitumia vibaya zaidi ya
shilingi 400,000 ambapo Aprili 3, mwaka huu alifikishwa polisi Kituo cha
Oysterbay, jijini Dar.
Mwandishi wetu alifika katika ofisi za Moan’s Drinks Ltd alikokuwa akifanyia kazi Mhindi huyo na kuonana na mmoja wa viongozi wa kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Raju na akakiri kutokea kwa kifo cha Talluri.
Habari zinasema mwili wake ulifanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jumatatu iliyopita na ukasafirishwa kupelekwa India Jumatano ya wiki iliyopita kwa ajili ya mazishi.

Kitanda walichokuwa wakilala wapenzi hao.
Mhindi huyo anadaiwa kuwa alikuwa mpenzi wa Mwalimu Elizabeth ambaye
siku moja kabla ya kifo chake imeelezwa kuwa alikuwa naye kwenye baa
moja karibu na nyumba ya Eliza, hata hivyo, alikutwa amekufa katika
chumba chake Kimara Baruti, Dar Aprili 15 mwaka huu huku shingoni kukiwa
na michubuko iliyoashiria kuwa alinyongwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, ACP Marietha Minangi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho katika hoteli hiyo.
“Ni kweli alikutwa amekufa katika Hoteli ya Transit na chumbani tulikuta sumu ambayo tumepeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi,” alisema.