Mtoto Farid Rashid mwenye umri wa mwaka 1 na miezi 8 anasumbuliwa na tatizo la kuziba kwa mirija inayosafirisha haja ndogo( mkojo) kati ya Figo na Kibofu cha mkojo. Baba Mzazi (Rashid Said) wa mtoto huyo anawaomba msaada wadau mbalimbali ili aweze kumpeleka mtoto Farid nchini India kwa matibabu zaidi.
“Mwanangu anajisaidia kwa maumivu makali, sema kweli ni mateso makubwa kwa mtoto, naomba mnisaidie mwanangu apate matibabu” hayo ni maneno ya baba mzazi wa Farid (Rashid Said).
Akizungumza na Msimamizi wa Mtandao wa habari wa MO BLOG Bi. Johari Kachwamba Ndugu Rashid Said amesema amemzungusha kwa matibabu mtoto Farid katika hospital mbalimbali za hapa nchini bila mafanikio ikiwa ni pamoja na kulazwa zaidi ya miezi mitatu(3) katika hospitali ya taifa ya Muhibili.
Katika juhudi za wazazi wa Farid kutafuta misada, wamefanikiwa kupata tiketi moja (1) ya ndege, dola 1,500 pamoja na Shilingi Milioni moja (1) lakini bado haitoshi.
Hata hivyo tayari wamefanikiwa kupata hati za kusafiria (Passport) na VISA ya nchini India ambayo inakoma (expire) 19-06-2012.
Hivyo anaomba msaada wa kupata tiketi nyingine pamoja na gharama za matibabu.
Nambari ya simu ya baba mzazi ni 0655-000556 au wasiliana na MO BLOG kupitia nambari 0714-940992.